JE QURANI INAAMURU WATU KUVUA VIATU WAKATI WA
IBADA?
NA MWALIMU ZABLON.
Utangulizi
Mara
nyingi sisi wakristo tumeshutumiwa sana na waislamu kwa kuto toa viatu wakati
wa lbada. Kuna vikundi vingi sana vya waislamu hasa waendeshaji mihadhara,
vikundi hivi vinazunguka sehemu mbalimbali wakifundisha watu kuwa nilazima watu watoe viatu wakati wa lbada, Kwani hata manabii wa zamani walifanya hivyo. Na
ukiwauliza ni wapi qurani inaamuru kutoa viatu wanakuwa wakali. Swali la
kujiuluza, je ni kweli au ni uongo. Fuatilia somo hili ili upate kufamu.
Al'Hajj 22:67 (kuhiji)
Kila
umma tumeujalia kawaida ya lbada wanayoishika. Basi wasishindane nawe katika
jambo hili. Na walinganie watu kwendea (Dini ya) Mola wako. Bila shaka wewe uko
juu ya uongozi uliosawa kabisa.
Kama
waslamu wangalijua maana ya aya hii, wasingalipiga makelele. Kwani Mungu wao
Allah anasema kuwa kila umma ameujalia kawaida ya lbada. Kwani kila umma una
lbada tofauti umma mwingine.
Sehemu
kuu ya somo hili
1. hoja za waislamu kuhusu
kutoa viatu.
2. Kwa nini musa na Yoshua wakatoa
viatu.
3. Je wakristo tumeamrishwa
kutoa viatu?
4. Je kuvua viatu ni lbada?
1. Hoja za waislamu kuhusu
kutoa viatu.
Waislamu hupenda kutumia hoja zifuatazo
kwa kudai kuwa zinahamrisha watu kuvua viatu wakati wa ibada.
Kutoka
3:4-6
Bwana
alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile
kijiti, akasema Musa! Musa! Akasema mimi hapa. Naye akasema, usikaribie hapa;
vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali usimamapo ni nchi takatifu. Tena
akasema mimi ni Mungu wa baba yako lbrahimu, Mungu wa lsaka, na Mungu wa
Yakobo. Musa akaficha uso wake maana aliogopa kumwangalia Mungu.
Andiko
lingine wanalolipotosha ni hili.
Yoshua
5:13-14
Ikawa
hapo Yoshwa alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho na kuangalia, na tazama
mtu mume akasimama akamkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi
mwake; Yoshwa akamwendea, na kumwambia, je! wewe uko upande wetu au upande wa
adui zetu? Akasema, la lakini nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la Bwana.
Yoshwa akapomoka kiusouso hata nchi akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia
nini mimi mtumishi wake? Huyo amiri wa jeshi la Bwana akamwambia Yoshwa, vua
viatu vyako miguuni mwako, kwa kuwa mahali hapo usimamapo ni patakatifu. Yoshua
akafanya vivyo.
Hapa
tunaona Musa na Yoshua waliambiwa watoe viatu vyao, swali kwako wewe muislamu
unaetoa viatu wakati wa lbada. Je ni aya gani katika Qurani au Biblia inayokupa
wewe ruhusa ya kutoa viatu, na kama hakuna amri hiyo mnatoa wapi au ni ibada za
kujitungia tu?
Wewe
kama mwislamu tafakari aya zifwatazo kwa makini ili upate kuelewa.
Zaburi
139:7-12
Niende wapi nijiepushe na
roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? Kama ningepanda mbinguni, wewe uko;
ningefanya kuzimu kitanda changu, wewe uko. Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na
kukaa pande za mwisho za bahari; huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono
wako wa kuume utanishika. Kama nikisema, hakika giza litanifunika, Na nuru
inizungukayo imekuwa usiku; giza nalo halikuchi kitu, Bali usiku huangaza kama
mchana; Giza na mwanga kwako ni sawaswa. (Pia tazama lsaya 6:3; Yeremia
23:23-24; Mithali 15:11)
Kwa
mjibu wa Biblia tunaona kuwa Mungu yuko kila mahali, kwani hatuwezi kujificha
uso wa Mungu.Hebu tuangalie jinsi Qurani inavyofundisha.
Al-an'am
6:3
Na yeye ndiye Mwenyezi Mungu
katika mbingu na katika ardhi, na anaijua ndani yenu na nje yenu; anayajua
(yote) mnayoyachuma.
Al
Baqarah 2:115
Na mashariki na magharibi ni
ya Mwenyezi Mungu. Basi popote mgeukiapo (alikokuamrisheni Mwenyezi Mungu
mtazikuta) huko radhi za Mwenyezi Mungu. Bila shaka mwenyezi Mungu ni Mwenye
wasaa (mkubwa kabisa) na mwenye kujua kukubwa (kabisa vile vile) (24:35)
Kwa
kuwa Mungu yuko kila mahali, naomba majibu kwa maswali fuatayo.
·
Je Musa na Yoshua waliweka wapi viatu vyao ambako hakuepo Mungu?
·
Na kama Musa na Yoshua walivishika mkononi, hakuwa najisi?
·
Je ni lini hio ibada ya kutoa vyatu ilihamia msikitini kutoka kichakani?
·
Kando na hawa kunae mwingine aliyeamurishwa kuvua viatu?
Kwa
hivyo muislamu kabla ya kuanza kuzungumza, ni lazima ujihoji kwa maswali hayo
hapo juu, na utaona ya kuwa Mungu hakuwa na maana kama waislamu
wanayoichukulia, kwani Mungu mwenyewe asema hivi.
Isaya
55:8
Maana mawazo yangu si mawazo
yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.
2.kwa nini Musa naYoshua
wakatoa viatu.
Biblia
inatufusha ya kuwa wamesimama katika inchi takatifu. Mungu alikuwa na maana ya
kujitakasa nafsi zao. Kwa mfano,
Walawi
11:44
Kwa kuwa mimi ni BWANA,
Mungu wenu; takaseni nafsi zenubasi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni
mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yoyote, kiendacho juu ya nchi. Kwa kuwa mimi ni BWANA niliyewaleta
kutoka katika nchi ya misri, ili kwamba niwe Mungu kwenu; mtakuwa watakatifu,
kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
Mungu
wetu mara nyingi hunena maneno ambayo katika hali ya mafumbo, na mtu ya mwili
hawezi kufahamu. Kama vile, Mungu ametuambia kuwa tuzitahi nyama govi ya roho
zetu wala tusiwe wenye shingo ngumu. kumbukumbu la torati 10:16; walawi 26:4;
Yeremia 4:4; wakolosai 2:11.mfano mingine wa kuangalia ni Ufunuo 2:7. Na mwenye
sikio na asikie….
3. Je wakristo wameamriswa
kutoa viatu?
Swala
la msingi la kuchunguza ni jinsi Biblia inavyofundisha kuhusu viatu.
Kutoka
12:11
Tena mtamla hivi, mtakuwa
mefunga viuno vyenu, mmevaa viatu miguuni na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi
mtamla kwa haraka ni pasaka ya Bwana.
Kulingana
na mafundisho ya Biblia hii ni lbada maluumu, na Mungu amesema kuwa watutakuwa
wamevaa viatu. Fuatilia somo hili ili upate kujua ukweli wa mambo.
Kumbukumbu
la torati 29:5
Nami miaka arobaini
nimewaongoza jangwani; nguo zenu hazikuchakaa juu yenu, wala kiatu chako
hakikuchakaa katika mguu wako.
Mungu
kwa miaka arobaini alikuwa akiwaongoza katika jangwa huku wamevaa viatu mguuni
mwao. Kwa hivyo tunaona jinsi Mungu alivyo mwingi wa rehema, kwani katika mila
na desturi za kiyahudi ni lazima kila mtu avae viatu. Na ndiposa nabii Yeremia
ansema hivi.
Yeremia
2:25
Zuia
mgu wako usikose kiatu, na koo yako isiwe na kiu…
Hata
Yohana kwa ushuhuda wake anasema maneno haya.
Mathayo
3:11
Kweli
mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana
nguvu kuniliko mimi, wala sisitahili hata kuvichukwa viatu vyake; yeye
atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na moto.
Kwa
wakristo Bwana Yesu ndiye mfano mwema, kwani yeye ndiye njia na kweli na uzima
mtu hawezi kumfikia Mungu bila bwana wetu Yesu kristo. Yohana 14:6.
Je
kunayo aya yoyote inayowaruhusu waislamu watoe viatu wakati wa ibada?.
Al-AHZAB
33:21
Bila shaka mnao mfano mwema (ruwaza nzuri) kwa mtume wa
Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na kutaja Mwenyezi Mungu sana.
Kwa
waislamu mfano wao mzuri ni mtume Muhammad, kwani alichokitenda inawapasa wao
kukitenda. Hebu tuangalie jinsi mtume alivyokuwa akisali, tukichunguza na
vitabu vingine. Kwa sababu Qurani inaruhu kusoma hata hadithi za mtume.
Ash-shura
42:10
Mkihitilafiana katika jambo lolote (rejeleeni kitabu cha
Mwenyezi Mungu na hadithi za mtume kwani) hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu.
Huyo Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu ninaye mtegemea, na kwake ninarejea.
Hivyo
kila mwislamu hata afanyenini ni lazima matamanio yake kama alivyotenda mtume.
Na mojawapo ya yale alioyatenda ni kusali huku amevaa viatu.
MISHKAT
AL MASABIH VOL 1 SURA (CHAPTER) 10 SEHEMU 3.
Mtume
alikuwa akisali huku amevaa viatu, Al Mughira alijaribu kumkumbusha Muhammad
hasa pale alipomwona anatawadha juu ya viatu na kuingia navyo msikitini, hivyo
Mughira akasema “Ewe Mtume wa Allah umesahau’’ Mtume akajibu kumwambia Al
Mughira akisema “wewe ndiwe uliye sahau kwa maana hivi ndivyo alivyo niamuru
Mungu.
Kama
mtume aliambiwa asali na viatu, mbona wewe mwislamu unatoa vyatu?. Je wewe
unamfuata nabii yupi?. Mafundisho ya kutoa viatu umeyapata wapi?
SAHIH
MUSLIM VOL 1 HADITHI 1127. UK 277.
Abdullah
bin Shakhkhir kuwa alikuwa akisali na mtume wa Allah, (katika msikitini) kisha
akamwona akitema mate na kuyafuta kwa kiatu.
Kunaruhusiwa
kusali huku umevaa viatu.
SAHIH
MUSLIMU VOL 1 HADITHI 1129
Sa’d
bin Yazid (Abu mslama) akimliza mtume Anas bin Malik. Je mtume wa Allah alikuwa
akisali na viatu vyake, Anas akajibu NDIYO.
IBADA
YA KWELI SI KUVUA VIATU BALI NI KUMUABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI BALI SI
KATIKA KUVUA VIATU.
Asiliana
name kupitia yesundiyenjia@hopefm.org
BARAKA!
No comments:
Post a Comment