KANISA
Kanisa ni
nini? Je Kanisa ni jengo? Je, ni mahali watu wanakusanyika ili kuabudu Mungu?
Au Kanisa ni watu-Waumini wanaomwamini na kumfata Yesu? Jinsi tunavyoelewa
kanisa ni kitu cha muhimu kwa kutusaidia kujua jinsi ya kuishi na kuenenda
katika imani yetu kuu.
Baadhi ya watu wanaamini kwamba neno
Kanisa limetajua mara ya kwanza na Bwana Yesu katika aya ifutayo:
Mathayo 16:16–18
Simoni Petro akajibu akasema wewe ndiwe Kristo mwana wa Mungu aliye hai Yesu akajibu akamwambia heri wewe Simon Bar Yona kwa sababu mwili na damu hazikukufunulia haya bali baba yangu aliye mbinguni nami nakuambia wewe ndiwe Petero na juu ya Mwamba huu nitalijenga kanisa langu wala milango ya kuzimu haitalishinda.”
Simoni Petro akajibu akasema wewe ndiwe Kristo mwana wa Mungu aliye hai Yesu akajibu akamwambia heri wewe Simon Bar Yona kwa sababu mwili na damu hazikukufunulia haya bali baba yangu aliye mbinguni nami nakuambia wewe ndiwe Petero na juu ya Mwamba huu nitalijenga kanisa langu wala milango ya kuzimu haitalishinda.”
Maana halisi ya kanisa
Neno “Kanisa” kama linavyo elezwa na
maandiko matakatifu, limetokana na neno la kigiriki ambalo ni ekklesia ambalo
maanake halisi ni “kusanyiko” na “kuwaita watu” au “wale ambao wameitwa” kwa
kifupi tu ni kwamba Kanisa ni mwili wa waumini ambao wameitwa au wamesikia
mwito kutoka ulimwenguni na Mungu ili waishi kama watu wake chini ya himaya au
mamlaka ya Kristo Yesu (Waefeso 1:22-23)
Baadhi ya maadui wa injili na hasa
waislamu mara nyingi hua wanauliza na kujenga maswali yasio faa juu ya Kanisa
ima kwa ujinga au kwa ujeuri tu ili ionekane kwamba Kanisa ni kitu hakipo au ni
kitu kisicho faa. Baadhi ya hoja wazijengazo kinyume na injili tukufu ni haya:
HOJA
ZA KANISA
1.
Wapi aya Yesu kaingia Kanisani?
2. Kanisa
imejengwa juu ya shetani Mathayo 16:8
3. Eti
Kanisa ni kiti cha enzi cha shetani Ufunuo 2:12-13.
4. Kanisa
ni nyumba ya kileo- Mithali 9:1
5. Kanisa
ni nyingi gani ndio bora?
6. Kanisa
ni nyumba ya mafarakano 1 Korinthians 11:7 (No place for disorder 1Cor 14:33).
Kanisa ni mwili wa Yesu Wakolosai 1:18, 1:24
Yesu ndiye kichwa cha Kanisa Waefeso 4:23
Tuko na Kanisa la ukweli na la uongo
Mfano wa kanisa la uongo 2 petero 2:1
Mfano wa Kanisa la ukweli ni gani? Waebrania 12:24
JINSI
YA KUKUA SEHEMU YA KANISA
Mtu hufanyika sehemu ya kanisa pale
anapo mkubali Bwana Yesu kukua Bwana na mwokozi wa maisha yake.
KUSUDI
KUU LA KANISA NI GANI?
Kusudi kuu la Kanisa lipo mara mbili
kwanza ni Kanisa huja pamoja (hukusanyika) na kusudi la kuhimizana na kujenga
katika masala ya kiroho ili mtu akomee (Waefeso 4:13). Kanisa hufikia na kusambaza
upendo na injili kuu ya Mbwana Yesu Kristo kwa wale wasio amini ulimwenguni
(Mathayo 28:18-20). Hii ndio iitwayo Mwito mkuu hivo basi kusudi la Kanisa ni
kuhudumia waumini na wasio waumini.
1 Wakorintho 12:27, Kanisa ni mwili mmoja
(Mw. ZABLON NYONJE).
No comments:
Post a Comment