Wednesday, 18 September 2013

TOFAUTI YA MTAZAMO WA NDOA NA WAKE KATIKA BIBLIA NA KURANI.



          NDOA NA UNYUMBA KATIKA BIBLIA NA KURANI/UISLAMU

Mungu aliweka ndoa kwa sababu tatu;
  1. Ushirika.
Mungu aliona si vyema kwa mtu kukua pekee yake
“Bwana Mungu akasema, si vyema huyo mtu awe peke yake, nitamtafutia msaidizi wa kufanana naye.” (Mwanzo 2:18).

  1. Ili familia na jamii kwa ujumla iweze kudhibitika kwa kukua na watoto.
“Mungu alimwambia mwanaume na mke, zaeni, mkaongezeke, mkaijaze inchi, na kuitiisha…” (Mwanzo 1:28).

  1. Kutoshelezana mahitaji ya kindoa (kingono).
“Kwa hivyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja, nao walikua uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona haya.” (Mwanzo 2:24-25).

Lakini kupitia dhambi Adamu na Hawa walianguka, utukufu ule ambao Mungu alikusudia ukawatoka, walitoka kwa mpango wa mbele wa Mungu.
Dhambi zao zikawafanya kutambua aibu zao na utengano kati yao, “Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.” (Mwanzo 3:7).
Mashtaka,
“Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.” (Mwanzo 3:12).
Na utawala wa Bwana juu ya mke
“Akamwambia mwanamke Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tama yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.” (Mwanzo 3:16). Zaidi,
Vitu vya asili havikukua chini ya utawala wao bali adui wao,
“Akamwambia Adamu, kwa kua umeskia sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nilikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbi utarudi.” (Mwanzo 3:17-19).

Haikuchukua muda mrefu saana kwa maovu mengine kutokea,

Baadhi yao
(I)Uuaji,
“Kaini akamwambia Habili nduguye [Twende uwandani].* Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua”. (Mwanzo 4:8)

(II)Kuoa wake wengi,
“Lameki akajitwalia wake wawili; jina la wa kwanza ni Ada, na jina la wa pili ni Sila.” (Mwanzo 4:19). Na,

(III)Kulipisha kisasi.
“Lameki akawaambia wake zake, sikieni sauti yangu, Ada na Sila;
Enyi wake za Lameki, sikilizeni usemi wangu; Maana nimemwua mtu kwa kunitia jeraha; kijana kwa kunichubua, Kama Kaini akilipiwa kisasi mara Saba, Hakika Lameki atalipiwa mara sabini na Saba.” (Mwanzo 4:23-24)

TALAKA IKAWA KAWAIDA
Sheria ya Musa ilihusisha  mielekezo au maagizo kupunguza mabaya yaliyo jitokeza kutokamana na ndoa ya wake wengi (Kutoka 21:10, Kumbukumbu 21:15-17)
Na Talaka, (Kumbu kumbu 24:1-4).
Lakini Mungu hakutaka habari za ndoa ya wake wengi ama talaka.
Tangu mwanzo Mungu alikusudia mtu abakie ameoleka kwa mke mmoja maisha yake yote.
“Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, akasema, kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakua mwili mmoja? Hata wamekua si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe. Wakamuambia, jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumuacha? Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu lakini tangu mwanzo haikuwa hivi, 9 Nami nawaambia ninyi, kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini”. (Mathayo19:4-9).

Ndoa kwa Wakristo ina umuhimu wakipekee kwa sababu inafananishua na umoja/ushirika uliopo kati ya Kristo na Kanisa lake, “Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa. Lakini kila mtu na ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe”. (Waefeso 5:32-33)

Wakati Bwana Yesu alitembea duniani, alibariki ndoa wakati wa muujiza wake wa kwanza/awali (Yohana 2:1-11), Yesu pia alitangaza mwanzo wa ufalme wa Mungu. Hivyo ni uhusiano mpya kati ya Bwana na Bibi.

Mtume Paulo anasema, “Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo  mmemvaa Kristo hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.” (Wagalatia 3:27-28). Hivyo basi waume kwa wake wako sawa machoni pa Mungu na katika ndoa pia.
Biblia inakubali kwamba mabwana na mabibi wote wako sawa katika maisha yao ya kindoa, Mtume Paulo anasema kwamba wanafaa kutoshelezana majukumu yao ya kindoa mmoja kwa mwingine (1Wakorintho 7:3-5). “Mume na ampe mkewe…
                NDOA KATIKA UISLAMU NA KURANI
Uislamu unakubali talaka, kuoa wake wengi na kutokua na usawa ndani ya ndoa.
Fatilia somo;
·         Wanaume wanaruhusiwa kufanya Talaka (2:230+fn)
·         Ooeni mtakavyo mmoja, wawili au watatu (S3:4)
·         Wanawake ni kama konde(yani shamba) basi ziendeeni mtakavyo, (Ngono ya nyuma na mbele) (S2:223).
·         Wapigeni wanawake mnao ona uasi kwao (4:34)
·         Watu wamepewa huba ya kupenda wake na mali (3:14)
·         Wanawake ni zawadi ya wanaume peponi (44:51-54, 78:31-33).
·         Wanawake na watoto ni maadui wa wanaume (S 64:14)

“The prophet said, “I stood at the gate of paradise and saw that the majority of the people who entered it were the poor, while the wealthy were stopped at the gate (for the accounts). But the companions of the fire were ordered to be taken to the fire. Then I stood at the gate of the fire and saw that the majority who entered it were women” (Bukhari vol. 7 Bk 62 no.124 pg 94)

*(Jesus will come as a bride to take his church; the church will be married to him).

Women, dogs and donkeys can annul the prayers of a man, according to Bukhari, vol. 1, Hadith 490 and 493. Compare with 1Peter3:7 Isaiah 59:1-2

No comments:

Post a Comment