MALAIKA GABRIEL NDIYE
JIBRIL?
Tokea kuanzishwa Kwa dini ya uislam, waislamu duniani
wanaamini na kuifundisha jamii kuwa malaika aitwae ‘Gabriel’ Kama maandiko
matakatifu ya Biblia yanavyofundisha ndiye malaika ‘Jibril’ Kama Quran
inavyosimulia. Swali la muhimu je ni kweli kuwa malaika “Gabriel” ndiye
“Jibril” nakusihi fuatilia somo hili ili kujua ukweli….
HOJA ZA WAISLAMU ZA KUAMINI KUWA MALAIKA GABRIEL NDIYE JIBRIL
Waislam wanalinganisha kwa kusoma aya za Quran na Biblia na
kusema kuwa malaika Gabriel ndiye Jibril wanasoma aya hizi….
QURAN 19:16-17 SURAT
MARYAM
16. Na mtaje Mariamu kitabuni (humu) alipojitenga na jamaa
zake (akenda) mahali upande wa mashariki (wa msikiti) 17. Na akaweka pazia
kujikinga nao.Tukampelekea muhuisha sharia yetu (jibril) - akajimithilisha
kwake kwa sura ya Binadamu aliye kamili.
LUKA 1:26-28
26. Mwezi wa sita, malaika Gabriel alitumwa na Mungu kwenda
mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti. 27. Kwa mwana mwali bikira aliyekuwa
ameposwa na mtu jina lake Yusufu wa mbari ya Daudi. Na jina lake Bikira huyo ni
Mariamu 28 Akaingia nyumbani kwake akasema, salamu uliyepewa Neema, Bwana yu
pamoja nawe.
“Mbali na kusoma aya hizi, pia wanaendelea kusoma kitabu cha
maisha ya nabii Muhammad kilichotungwa na aliyekuwa kadhi mkuu wa Kenya marehemu
sheikh Abdallah Saleh Al-Farsy katika ule ukurasa wa 17 kifungu (A) kuna maneno
haya...
NAMNA YA KULETWA
WAHYI…
Waislamu wanaitikadi kuwa Quran ni maneno ya Mwenyezi Mungu
na vilevile Taurat ya nabii Musa na injili ya nabii Isa, na Zaburi ya nabii
Daudi. Vyote pia ni vitabu vyenye maneno ya mwenyezi Mungu. Lakini Mungu
haonekani Kwa macho wala hayupo mahali mahsusi. Basi vipi hao mitume wamepata
maneno haya? Jawabu yake ni hii wao huyapata ima kwa Jibril malaika mkubwa kuliko malaika wote wa Mwenyezi Mungu.
QU-RAN 53:2-6 SURATUL
NAJM (NYOTA)
2. Kwamba mtu wenu huyu Nabii Muhamad (hakupotea Kwa ujinga)
na wala hakukosa (na hali ya kuwa anajua) 3. Wala hasemi Kwa matamanio (ya
nafsi yake) 4. Hayakuwa haya (anayosema) ila ni wahyi (ufunuo) uliofunuliwa
(kwake) 5. Amemfundisha (malaika) mwenye nguvu Sana 6. Mwenye uweza na yeye
(huyu jibril) akalingana sawa sawa.
Waislamu kwa kusoma aya hizi, wanaamini Malaika Gabriel
ndiye jibril lakini aya hizi zinaonyesha tofauti kwani malaika Jibrili
alipelekwa na Allah aende kwa Mariamu ambaye alikua msikitini na Quran
haikutaja mji wala nchi aliyoenda jibril, lakini tunaona Biblia inafundisha
kuwa, malaika Gabriel aliingia nyumbani kwa Mariamu na tena biblia
inatufundisha kuwa ufunuo wa unabii uliletwa kwa muongozo wa Roho Mtakatifu (2 Petro 1:20-21) na wala si malaika
jibril kama Qurani inavyosimulia.
JE, MALAIKA NI VIUMBE
WA NAMNA GANI?
WAEBRANIA 1:13-14.
13. Je, yuko malaika aliyemwambia wakati wowote uketi mkono
wangu wa kuume hata nitakapo waweka adui zako chini ya nyayo zako? 14. Je, hao
wote si “roho”watumikao walitumwa kuwahudumu wale watakao urithi wokovu?
Ni wazi tunaona kuwa malaika ni vyumbe ambao ni nafsi ya
roho ambao wanauwezo wa kuwajia watu kwa umbo la wanadamu eg (Mwanzo
18:1-19:12) kama tunavyoona walipomwendea Ibrahim na lutu.Malaika alimwendea
Musa katika sura ya kijiti kinacho waka bila kuteketea (kutoka 3:1-5)
JE, MALAIKA WOTE NI
WEMA NA HAWAMKOSEI MUNGU?
Tukisoma Quran tunaona Allah Mungu anayeabudiwa na waislamu
anasimulia malaika kuwa ni viumbe wenye sifa hii.
QURANI 16:93 SURATUL
AL-NAHL (NYUKI)
Na Mwenyezi Mungu angalitaka kwa yakini angalikufanyeni
“kundi moja tu” (mnamtii nyote kama alivyowafanya “malaika” lakini kakuachieni
mfanye mtakavyo) lakini anamuachia kupotea anayemtaka na anamuongoa anayemtaka
na hakika mtaulizwa kwa yale mliokuwa mkifanya.
QUR-AN 32:13 SURAT
AS-SAJDAH (KUSUJUDU)
Na tungalitaka tungempa kila mtu uwongofu wake (Kwa lazima Kama
tulivyowapa malaika…..
UFAFANUZI WA AYA YA
13 ULIO NDANI YA QUR-AN NI HUU…
Angetaka mwenyezi Mungu angemuumba Binadamu Kama malaika
hawezi kufanya mabaya, maumbile yake ni kufanya mema tu; kwa hiyo halipwi kwa
mema yake hayo kwani hayaonei taabu katika kufanya. Lakini binadamu ameumbwa Kwa
uweza wa yote mawili sawasawa na raha yake zaidi ni kufanya mabaya.
Kadiri ya aya hizi Allah Mungu anayeabudiwa na waislamu
anasema kuwa malaika ni wema na hawawezi kufanya mabaya na wako kundi moja tu
na wote wanamtii Allah. Lakini tukirejea kwa Biblia tunaona Mungu wetu Jehovah
amefunulia mitume wake kuwa malaika wako hivi…
2PETERO 2:4
Kwa maana Mungu hakuwaachia “malaika waliokosa” bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo
vya giza walindwe hata ije siku ya hukumu.
Hao malaika waliokosa wapo chini ya ibilisi, mbali na hao
waliokosa lakini pia wapo malaika wa namna hii…
MATHAYO 25:31
Hapo atakapokuja mwana wa adamu, katika utukufu wake na
malaika watakatifu wote pamoja naye; ndipo atakapo keti katika kiti cha utukufu
wake.
Kadri ya aya hizi tunaona wazi wazi kuwa Mungu wetu
anafundisha makundi mawili ya malaika, wema (yaani Watakatifu) na wabaya (yaani
waliokosa) Fundisho ambalo Allah halielezei kwani yeye Allah anasema malaika ni
wema tu hawawezi kufanya mabaya “hali hii inatufundisha kuwa Allah siyo
Yehova”.
MAANA YA NENO GABRIEL
Neno au jina “Gabriel” asili yake ni lugha ya kiebrania na
maana ni “Mjumbe wa Mungu” katika Biblia jina hili Gabriel limetajwa mara “nne”
(4) (Tazama Danieli 8:16 na 9:21, Luka 1:19 na 1:26) kuhusu malaika Gabriel
mara nyingi Biblia inaonyesha kuwa Mungu anamtuma ili alete habari njema
zinazohusu wokovu wa wanadamu na hutoa maneno ya kuwafariji wale aliowatokea
akisema “usiogope”katika Biblia limetajwa mara (366) aidha tunaposoma Biblia
tunaona pia malaika huyu anaitwa malaika wa Bwana (The angel of the Lord) Neno
hili katika biblia limetajwa mara (65) katika aya zipatazo (61) iwapo sehemu
hizo zote zinahusika na malaika Gabriel basi malaika huyo atakuwa ametajwa mara
nyingi.
NAMNA YA KUJUA TOFAUTI
YA MALAIKA GABRIEL NA JIBRIL
1 TIMOTHEO 4:1
Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine
watajitenga na imani WAKISIKILIZA
roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani.
(Tazama pia Mathayo 7:15-20)
1YOHANA 4:1, 3, 15
1. Wapenzi msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho,
kwamba zimetokana na Mungu; Kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani
3. Na “kila roho isiyomkiri Yesu” haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya
mpinga Kristo, ambayo mmeisikia kwamba yaja, na sasa imekwisha kuwako duniani
15. Kila akiriye ya kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake naye
ndani ya Mungu.
Jambo la muhimu ni la kujaribu kati ya jibril na Gabriel ni
nani aliye mkiri Yesu kuwa ni Mwana wa MUNGU endapo fundisho lao ni moja basi
pia watakuwa siyo malaika wawili bali mmoja- wakitofautiana itakuwa siyo mmoja
bali ni malaika wawili walio tofauti kabisa..
JE, CHEO CHA MALAIKA
GABRIEL NI SAWA NA JIBRIL?
MALAIKA GABRIEL ALIYETUMWA NA MUNGU YEHOVA ANASEMA HIVI…
Malaika akajibu akamwambia Mimi ni Gabriel, nisimamaye mbele
za Mungu, nimetumwa niseme nawe na kukupasha habari hizi njema (Tazama Luka
1:19)
Kwa mujibu wa ayah ii malaika Gabriel anaeleza kuwa husimama
mbele za Mungu hivyo ni wazi kuwa cheo chake ni mjumbe asimamaye mbele ya
Mungu. Je, malaika jibril anayetumwa na Mungu aitwaye Allah cheo chake ni hiki
hiki cha Gabrieli?
QURAN 81:19-21 SURATUL
AT-TAKWIR (JUA LITAKAPO KUNJWA KUNJWA)
19. Kwa hakika
hii (Qurani) ni kauli aliyo kuja nayo mjumbe mtukufu (jibril) 20. Mwenye nguvu, mwenye cheo cha
heshima kwa Mwenyezi Mungu 21.
Anayeitiiwa huko (mbinguni na malaika wenziwe) kasha mwaminifu.
UFAFANUZI WA AYA YA
19-21 ULIO NDANI YA QUR-AN NI HUU…
Mjumbe mtukufu na mwenye kutiiwa huko mbinguni ni “jibril”
ambaye ndiye “mkubwa wa malaika wote.”
JE, MALAIKA MKUU WA YEHOVA NI NANI?
YUDA 1:9 “Lakini
Mikael malaika “mkuu” aliposhindana na Ibilisi….. Katika ayah ii tunaona Mungu
wetu tunayemwabudu wakristo aitwae Yehova malaika wake mkuu ni Mikaeli na Mungu
anayeabudiwa na waislamu aitwaye Allah malaika wake mkuu ni Jibril. Hivyo
Jibril siyo Gabriel. Tukirejea kwa malaika mkuu “Michael” hili ni jina lenye
asili ya lugha ya “kiebrania” na maana yake ni “Nani sawa na Mungu” hii kwa
sababu ndiye aliyewaongoza malaika wenziwe kumpiga shetani na kumtoa kule
mbinguni pale alipojikweza na kutaka kufanana na Mungu (Tazama Ufunuo 12:7-12
na Danieli 10:13,21na12:2)
MAFUNDISHO YAO KUHUSU
UWANA WA MUNGU
(A) MALAIKA
GABRIEL WA MUNGU YEHOVA ALIFUNDISHA HIVI..
LUKA 1:26-35 Nanukuu aya ya 35 tu
Malaika akajibu akamwambia, Roho
Mtakatifu atakujilia juu yako na nguvu zake aliye juu zitakufunika kama kivuli.
Kwa sababu hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu “Mwana wa Mungu”
(B) MALAIKA
JIBRIL WA MUNGU AITWAYE ALLAH ANASEMA HIVI…
QURAN 18:4-5 SURATUL AL-KAHF
(PANGO)
4. Na kiwaonye wale wanaosema
“mwenyezi Mungu amejifanyia mtoto 5. Wala hawana ilimu juu ya (jambo) hili wala
Baba zao (hawana ujuzi juu ya jambo hili ila wanajisemea tu) Ni neno kubwa hilo
litokalo katika vinywa vyao hawasemi ila uwongo tu
Maneno haya aliyafundisha malaika
jibril (QURAN 53:5-6) ni ya
kumkufuru Mungu wetu Yehova (Tazama kutoka
4:22) Mungu anasema “Israeli ni Mwanangu Mimi” na malaika wake Gabriel,
alifundisha uwana wa Mungu.
MAFUNDISHO YAO KUHUSU ROHO MTAKATIFU
LUKA 1:34-35 “Malaika Gabriel anamwambia Mariam hivi…
34. Mariam akamwambia malaika
litakuaje neno hili maana sijui mume? 35. Malaika akajibu akamwambia Roho
mtakatifu atakujilia juu yako na nguvu zake aliye juu zitakufunika kama kivuli-
Roho Mtakatifu ni Mungu (Matendo 5:3-4) Na wala siyo malaika ndio maana malaika
alisema atakujilia.
QUR-AN 16:102 SURATUL AL-NAHL (NYUKI)
Sema Roho Takatifu yaani jibril
ameiteremsha kutoka kwa mola wako kwa haki ili kuwathubutisha wale walio amini…
QUR-AN 2:87 SURATUL AL-BAQARAH (NG’OMBE)
Na hakika tulimpa Musa kitabu na
tukawafundisha mitume (wengine) Baada yake na tukampa Isa mwana wa Mariam hoja
zilizo waziwazi na tukamtia nguvu kwa roho mtakatifu (jibril)
UFAFANUZI WA AYA YA 87 ULIO NDANI YA QURAN NI HUU
Kwa waislamu Roho mtakatifu ni
“Malaika Jibril” si Yule wanaodai wakristo kuwa ni mmoja wa asili ya utatu
(Trinity). Hapa tunaona malaika Gabriel hasemi kuwa yeye ndiye Roho Mtakatifu
mahala popote lakini Jibril anasema eti, ndiye roho mtakatifu- hivyo Gabriel
siyo Jibril.
JE, MALAIKA JIBRIL ALIPELEKA UTUME KWA WAYAHUDI?
QUR-AN 2:97 SURATUL AL-BAQARAH (NG’OMBE)
Sema anayemfanyia ushinde jibril
kwa kuwa ndiye aliyemletea utume nabii Muhammad (asiwapelekee wayahudi) (ni
bure hana kosa Jibril) hakika yeye aliteremsha Quran moyoni mwako kwa idhini ya
Mwenyezi Mungu.
UFAFANUZI WA AYA YA 97 ULIO NDANI YA QUR-AN NI HUU...
“Mayahudi katika hila zao za
kumkataa mtume Muhammad walimwuliza “malaika gani anayekuletea wahyi? Mtume
akasema “Jibril” wakasema “Lo! HUYO NI ADUI YETU, HATUMTAKI lau kuwa malaika
mwingine ndiye anayekuletea wahyi (yaani ufunuo) tungekufuata. Jibrili
hajapeleka utume Kwa wayahudi; Isitoshe malaika huyo Jibril anafundisha kuhusu
wayahudi hivi….
QUR-AN 5:82 SURATUL AL-MAIDAH.
(MEZA YA CHAKULA)
“Hakika utawakuta walio “maadui”
zaidi kuliko watu (wengine) kwa waislam ni “mayahudi” Na wale mushirikina.”
Hapa tunaona Jibril anawafundisha
waislamu kuwa maadui zao zaidi ni wayahudi. Kuwa adui wa wayahudi ni kuwa adui
wa wokovu kwani Bwana Yesu anatufundisha hivi...
YOHANA 4:19-22 Nanukuu aya ya 22
tu
Ninyi mnaabudu msicho kijua, sisi
tunaabudu tukijuacho kwa kuwa, “wokovu watoka kwa wayahudi.”
Isitoshe manabii wote ni wayahudi
kutoka kwa Musa, Daudi, Isaya, Ezekieli, Daniel, Hosea, Mika, Malaki, Yohana
mbatizaji na hata Yesu.
JE, NAMNA MALAIKA GABRIEL ANAVYOTOKEA WATU NI SAWA NA JIBRIL?
(A) JIBRIL
QUR-AN 19:16-26
16. Na mtaje Mariam kitabuni (humu)
alipojitenga na jamaa zake (akenda) mahali upande wa (mashariki wa msikiti) 17.
Na akaweka pazia kujikinga Nao. Tukampelekea muhuisha sharia yetu (jibril) -
akajimithilisha kwake (Kwa sura ya) binadamu aliye kamili 18. (Mariamu) akasema
hakika Mimi najikinga kwa (Mwenyezi Mungu) mwingi wa rehema aniepushe nawe.
Ikiwa unamuogopa Mungu (basi ondoka nenda zako) 19. (Malaika) akasema hakika
mimi ni mjumbe wa mola wako ili nikupe mwana mtakatifu 20. Akasema nitawezaje
kupata motto, hali hajanigusa mwanamume (yeyote Kwa njia ya halali) wala mimi
si (mwanamke) mwenye kuzini 21. (Malaika) akasema ni kama hivyo( unavyosema
lakini mola wako amesema haya ni sahali kwangu ili tumfanye muujiza kwa
wanadamu na rehema itokayo kwetu (ndio tumefanya hivi) na hili ni jambo
lililokwisha kuhukumiwa 22. Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka
mahali pa mbali 23. Kisha uchungu ukampeleka katika shina la mtende (akawa
anazaa na huku) anasema,”laiti ningekufa kabla ya haya ningekua niliye
sahaulika kabisa 24. Mara ikamfikia sauti kutoka chini yake (inamwambia) “
usihuzunike hakika mola wako amejalia
(ameweka) kijito cha maji chini yako 25. Na litikise kwako shina la mtende
litakuangushia tende nzuri zilizo mbivu 26. Basi ule na unywe na litue jicho
lako.
JINSI JIBRIL
ALIVYOFANYA ALIPOMTOKEA MUHAMMAD NI HIVI…
Hata siku moja- katika mwezi wa Ramadan
mwezi 17 jumatatu katika mwaka wa 40
unusu wa umri wake- Mtume alimuona mtu kasimama mbele yake bila kumwona wapi
katokea, akamwambia,”soma” mtume akamjibu “Mimi sijui kusoma “kwani sijapata kujifundisha kusoma –“Akaja akamkamata” akambana,akamwambia
tena “soma” Mtume akamjibu jawabu yake ile ile.Hata mara ya tatu akamwambia tena “soma –igraa Bismi rabbik” akamsomea sura hiyo ya 96 mpaka kati yake
kasha mtume akaisoma kama alivyosomewa.Hii ndiyo sura ya kwanza kushuka katika
kurani. Ingawa haijawekwa mwanzo. Mara Yule mtu (malaika) akaondoka machoni
mwake-asimuone kenda wapi. Na mtume naye akarejea kwake-khofu ikamshika.
Alipofika nyumbani bibi Khadija alidhani ana homa, akamfunika manguo gupi gupi
na akakaa mbele yake akamsikiliza anavyoweweseka. Hata homa ilipomwachia
alimweleza Bibi Khadija yote yaliyomtokea na Bibi Khadija akamtuliza
moyo.Akamyakinisha ya kuwa hapana lolote baya litakalomzukia. Mara bibi huyu
akaondoka akenda kwa jamaa yake-Bwana Waraga Bin Naufal-akampa habari yote
iliyompata mumewe; naye akamwambie amwite, na mtume akenda akamweleza habari
yake yote. Bwana Waraga akamwambia “huyo ndiye Jibril aliyemshukia Nabii Musa
na Nabii Isa... Basi jibashirie kuwa wewe ni Mtume wa umma huu. Nami natamani kuwa
hai nikuone unavyosimama kuwatengeneza jamaa zako inshallah nitakuwa mkono wako
wa kulia wakarejea kwao na hofu yote imemtoka.
Habari hii inapatikana katika kitabu cha maisha ya Nabii Muhammad
(S.a.W) mtungaji ni Sheikh Abdulla Saleh Farsy aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar
baadaye akawa Kadhi Mkuu wa Kenya, katika ukurasa wa 16-17
12. KUJA UTUME (Page 12).
Hata siku moja katika mwezi wa
Ramadhan na hali ya kuwa mtume kasha timiza miaka 40 mara siku hiyo jibril
alimdhihirikia na kumjuvya kuwa kishakuwa Nabiy. Na vituko vingi alimfanyia kama tunavyosikia.
Basi mtume akafanya khofu akarejea
kwa mkewe akamhadithia; na pale pale homa
kubwa kabisa ikampanda akataka afunikwe maguo. Mara akawa anatetemeka kwa
nderema na anaweweseka na kusema “Najihofia
nafsi yangu kuchezewa na mashetani na kuniharibu akili yangu na kunizuga”. Bibi
Khadija pale pale alimdakiza akamwambia: Wacha hayo: siyo yatakuwa hayo. Wewe
huwezi kuchezewa na mashetani. Shetani hawezi kumchezea mtu mwenye sifa zako.
Wewe unatazama vyema jamaa zako, unachukua mizigo ya hata watu wasiokuwa wako.
Unawadhihirishia watu sifa nzuri ambazo hakuna mwenye anazo. Unafanya hivi na
unafanya hivi. Furahi ndugu yangu. Tua moyo wako. Wallahi! Mimi naona umeshakuwa mtume”.
Mnamsikia bibi huyu? Mke mama
Habari hii inapatikana katika kitabu kiitwacho Wakeze mtume wakubwa na
wanawe, mtungaji Sheikh Abdalla Saleh Farsy aliyekuwa Kadhi mkuu wa Kenya,
kimetangazwa na kuchapwa na ADAM TRADERS MOMBASA KENYA.
The arabs had faith in the existence of evil spirits whom they would
conjure up in solitary places they believed in sooth sayers and fortune tellers
and had implicit faith in their utterances (Al Hadis by Alhaji Maulana Fazlul
karim page 90)
(B)
MALAIKA
GABRIEL ALIVYOWATOKEA WATU ALIFANYA HIVI…
LUKA 1:19 Alijitambulisha Kwa kusema, “Mimi ni Gabriel.”
DANIEL 8:15-16 Au muhusika
ambaye alimtokea hujulishwa kwanza
DANIEL 8:17-21
LUKA 1:13, 30…
Gabriel anamsadia mtu pale
anapopatwa na hofu na anasema usiogope. Tabia za malaika Gabriel ni huruma na
kumfahamisha mtu kwa upole, lakini malaika Jibril wa Allah yeye hukamata,
kumbana mtu, jambo lililompelekea Muhammad apate homa. Swali je, huyo jibril ni Nani?
JE, ALLAH MUNGU WA WAISLAMU
ANAWATUMA VIUMBE GANI?
QUR-AN 19:83 SURATUL MARYAMU.
Je, huoni yakwamba tumewatuma
mashetani juu ya makafiri
wanaowachochea (kufanya mabaya) “Na namna hii tumemfanyia kila Nabii maadui
(Nao ni) mashetani katika watu na (mashetani katika) majini. Baadhi yao
wanawafunulia wenzi wao maneno ya kupambapamba ili kuwadanganya. (QUR. 6:112 suratul Al-An’am) SHETANI ANA
UWEZO WA KUJIGEUZA AWE MFANO HUU… 2WAKORINTHO 11:10-15, NA NUKUU AYA YA 14 TU “Wala
si ajabu maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa Malaika wa nuru.”
“Kila akiriye kuwa Yesu Ni Mwana WA Mungu, Mungu hukaa ndani yake, tena
roho ya kukiri hivyo imetoka kwa Mungu (1 Yoh 4:1-3, 15). Malaika Gabriel
amekiri kuwa Yesu Ni mwana WA Mungu, Jibril hakukiri hivyo “Luka 1:35” (Qur.
9:30). Je, Jibril ni nani?
NINI MWISHO WA VIUMBE HIVYO ANAVYOVITUMA ALLAH
Allah hutuma mashetani, maandiko
matakatifu ya Biblia yanatufundisha mwisho wa viumbe hao hivi;
MATHAYO 25:41 “Bwana Yesu atawaamuru hivi…
Kisha atawaambia na wale walioko
mkono wake wa kushoto, ondokeni kwangu mliolaaniwa; mwende, katika moto wa
milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake.
Ndugu mpendwa ni matumaini yangu
katika BWANA WETU YESU KRISTO kuwa
umeweza kujua wazi wazi kuwa Malaika Gabriel wa Mungu wetu Yehova siyo malaika
Jibril wa Mungu aitwaye Allah anayeabudiwa na waislamu BWANA akubariki Sana ueneze ujumbe huu kwa watu wa mataifa ili
wamgeukie Bwana Yesu wapate kuokolewa. Amina!
Kwa maswali au mawasiliano nasi
Tuandikie Kwa barua pepe yesundiyenjia@hopefm.org
No comments:
Post a Comment