KUTUHUSU

Yesu ndiye njia ni blog ambayo inajibu maswali ambayo waislamu huuliza wakristo.
Tunafanya huduma ya Yesu Kristo kwa utukufu wa Mungu mwenyewe, kwa kuitetea imani ya Kristo yaani Injili, mafundisho yake dhabiti kama vile Maandiko matakatifu yasemavyo na kanuni zake. Kufanya hivyo, Yesu ndiye njia huchambua mafundisho ya dini zingine kama vile Uislamu na mafundisho yake kinyume na ukristo na kufananisha na maandiko matakatifu. Kwa uchambuzi huo wote tunatumia Biblia kama chombo kikuu cha kukemea mafundisho mapotovu.
Unaweza kutuskiza kila siku ya ijumaa kwenye radio ya 93.3 hopefm-Nairobi, 93.9 hopefm Nakuru na magharibi mwa Kenya, 101.9 hopefm Mombasa na viunga zake, kuanzia saa Mbili ya jioni hadi saa inne.
Unaweza kutupata pia kwa mtandao yaani internet kwa www.hopefm.org na pia kwa ukurasa wa facebook, Yesu ndiye njia vilevile unaweza asiliana nasi tunapo endelesha kipindi kwa kutuma arafa yaani (sms).