Utangulizi
Mara nyingi sisi wakristo tumeshutumiwa
sana na waislamu kwa kuto toa viatu wakati wa lbada. Kuna vikundi vingi sana
vya waislamu hasa waendeshaji mihadhara, vikundi hivi vinazunguka sehemu
mbalimbali wakifundisha watu kuwa nilazi watu kutoa viatu wakati wa lbada,
Kwani hata manabii wa zamani walifanya hivyo. Na ukiwauliza ni wapi qurani
inaamuru kutoa viatu wanakuwa wakali. Swali la kujiuluza, je ni kweli au ni
uongo. Fuatilia somo hili ili upate kufamu.
Al'Hajj
22:67 (kuhiji)
Kila umma tumeujalia kawaida ya lbada
wanayoishika. Basi wasishindane nawe katika jambo hili. Na walinganie watu
kwendea (Dini ya) Mola wako. Bila shaka wewe uko juu ya uongozi uliosawa
kabisa.
Kama waslamu wangalijua maana ya aya hii,
wasingalipiga makelele. Kwani Mungu wao Allah anasema kuwa kila umma ameujalia
kawaida ya lbada. Kwani kila umma una lbada tofauti umma mwingine.
Sehemu kuu ya somo hili
1. hoja
za waislamu kuhusu kutoa viatu.
2. Kwa
nini musa na Yoshua wakatoa viatu.
3. Je
wakristo tumeamrishwa kutoa viatu?
4. Je
kuvua viatu ni lbada?
1.
Hoja za waislamu kuhusu kutoa viatu.
Waislamu
hupenda kutumia hoja zifuatazo kwa kudai kuwa zinahamrisha watu kuvua viatu
wakati wa ibada.
Kutoka 3:4-6
Bwana alipoona ya kuwa amegeuka ili
atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema Musa! Musa!
Akasema mimi hapa. Naye akasema, usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni
mwako; maana mahali usimamapo ni nchi takatifu. Tena akasema mimi ni Mungu wa
baba yako lbrahimu, Mungu wa lsaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akaficha uso wake
maana aliogopa kumwangalia Mungu.
Andiko lingine wanalolipotosha ni hili.
Yoshua 5:13-14
Ikawa hapo Yoshwa alipokuwa karibu na mji
wa Yeriko, akavua macho na kuangalia, na tazama mtu mume akasimama akamkabili
mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshwa akamwendea, na
kumwambia, je! wewe uko upande wetu au upande wa adui zetu? Akasema, la lakini
nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la Bwana. Yoshwa akapomoka kiusouso hata
nchi akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi wake? Huyo
amiri wa jeshi la Bwana akamwambia Yoshwa, vua viatu vyako miguuni mwako, kwa
kuwa mahali hapo usimamapo ni patakatifu. Yoshua akafanya vivyo.
Hapa tunaona Musa na Yoshua waliambiwa watoe
viatu vyao, swali kwako wewe muislamu unaetoa viatu wakati wa lbada. Je ni aya
gani katika Qurani au Biblia inayokupa wewe ruhusa ya kutoa viatu, na kama
hakuna amri hiyo mnatoa wapi au ni ibada za kujitungia tu?
Wewe kama mwislamu tafakari aya zifwatazo
kwa makini ili upate kuelewa.
Zaburi 139:7-12
Niende
wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? Kama ningepanda
mbinguni, wewe uko; ningefanya kuzimu kitanda changu, wewe uko. Ningezitwaa
mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari; huko nako mkono wako
utaniongoza, Na mkono wako wa kuume utanishika. Kama nikisema, hakika giza
litanifunika, Na nuru inizungukayo imekuwa usiku; giza nalo halikuchi kitu,
Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawaswa. (Pia tazama
lsaya 6:3; Yeremia 23:23-24; Mithali 15:11)
Kwa mjibu wa Biblia tunaona kuwa Mungu yuko
kila mahali, kwani hatuwezi kujificha uso wa Mungu.Hebu tuangalie jinsi Qurani
inavyofundisha.
Al-an'am 6:3
Na
yeye ndiye Mwenyezi Mungu katika mbingu na katika ardhi, na anaijua ndani yenu
na nje yenu; anayajua (yote) mnayoyachuma.
Al Baqarah 2:115
Na
mashariki na magharibi ni ya Mwenyezi Mungu. Basi popote mgeuliapo
(alikokuamrisheni Mwenyezi Mungu mtazikuta) huko radhi za Mwenyezi Mungu. Bila
shaka mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa (mkubwa kabisa) na mwenye kujua kukubwa
(kabisa vile vile) (24:35)
Kwa kuwa Mungu yuko kila mahali, naomba
majibu kwa maswali fuatayo.
·
Je Musa na Yoshua waliweka wapi
viatu vyao ambako hakuepo Mungu?
·
Na kama Musa na Yoshua walivishika
mkononi, hakuwa najisi?
·
Je ni lini hio ibada ya kutoa vyatu
ilihamia msikitini kutoka kichakani?
·
Kando na hawa kunae mwingine
aliyeamurishwa kuvua viatu?
Kwa hivyo muislamu kabla ya kuanza
kuzungumza, ni lazima ujihoji kwa maswali hayo hapo juu, na utaona ya kuwa
Mungu hakuwa na maana kama waislamu wanayoichukulia, kwani Mungu mwenyewe asema
hivi.
Isaya 55:8
Maana
mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.
2.kwa
nini Musa na Yoshua wakatoa viatu.
Biblia inatufusha ya kuwa wamesimama katika
inchi takatifu. Mungu alikuwa na maana ya kujitakasa nafsi zao. Kwa mfano,
Walawi 11:44
Kwa
kuwa mimi ni BWANA, Mungu wenu; takaseni nafsi zenubasi; iweni watakatifu, kwa
kuwa mimi ni mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha
aina yoyote, kiendacho juu ya nchi. Kwa
kuwa mimi ni BWANA niliyewaleta kutoka katika nchi ya misri, ili kwamba niwe
Mungu kwenu; mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
Mungu wetu mara nyingi hunena maneno ambayo
katika hali ya mafumbo, na mtu ya mwili hawezi kufahamu. Kama vile, Mungu
ametuambia kuwa tuzitahi nyama govi ya roho zetu wala tusiwe wenye shingo
ngumu. kumbukumbu la torati 10:16; walawi 26:4; Yeremia 4:4; wakolosai
2:11.mfano mingine wa kuangalia ni Ufunuo 2:7. Na mwenye sikio na asikie….
3.
Je wakristo wameamrishwa kutoa viatu?
Swala la msingi la kuchunguza ni jinsi
Biblia inavyofundisha kuhusu viatu.
Kutoka 12:11
Tena
mtamla hivi, mtakuwa mefunga viuno vyenu, mmevaa viatu miguuni na fimbo zenu
mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka ni pasaka ya Bwana.
Kulingana na mafundisho ya Biblia hii ni lbada maluumu, na Mungu amesema kuwa watutakuwa wamevaa viatu. Fuatilia somo hili ili upate kujua ukweli wa mambo.
Kumbukumbu la torati 29:5
Nami
miaka arobaini nimewaongoza jangwani; nguo zenu hazikuchakaa juu yenu, wala
kiatu chako hakikuchakaa katika mguu wako.
Mungu kwa miaka arobaini alikuwa
akiwaongoza katika jangwa huku wamevaa viatu mguuni mwao. Kwa hivyo tunaona
jinsi Mungu alivyo mwingi wa rehema, kwani katika mila na desturi za kiyahudi
ni lazima kila mtu avae viatu. Na ndiposa nabii Yeremia ansema hivi.
Yeremia 2:25
Zuia mgu wako usikose kiatu, na koo yako
isiwe na kiu…
Hata Yohana kwa ushuhuda wake anasema
maneno haya.
Mathayo 3:11
Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya
toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuniliko mimi, wala sisitahili hata
kuvichukwa viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na moto.
Kwa wakristo Bwana Yesu ndiye mfano mwema,
kwani yeye ndiye njia na kweli na uzima mtu hawezi kumfikia Mungu bila bwana
wetu Yesu kristo. Yohana 14:6.
Je kunayo aya yoyote inayowaruhusu waislamu
watoe viatu wakati wa ibada?.
Al-AHZAB 33:21
Bila
shaka mnao mfano mwema (ruwaza nzuri) kwa mtume wa Mwenyezi Mungu na siku ya
mwisho, na kutaja Mwenyezi Mungu sana.
Kwa waislamu mfano wao mzuri ni mtume
Muhammad, kwani alichokitenda inawapasa wao kukitenda. Hebu tuangalie jinsi
mtume alivyokuwa akisali, tukichunguza na vitabu vingine. Kwa sababu Qurani
inaruhu kusoma hata hadithi za mtume.
Ash-shura 42:10
Mkihitilafiana
katika jambo lolote (rejeleeni kitabu cha Mwenyezi Mungu na hadithi za mtume
kwani) hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Huyo Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu
ninaye mtegemea, na kwake ninarejea.
Hivyo kila mwislamu hata afanyenini ni
lazima matamanio yake kama alivyotenda mtume. Na mojawapo ya yale alioyatenda
ni kusali huku amevaa viatu.
MISHKAT
AL MASABIH VOL 1 SURA (CHAPTER) 10 SEHEMU 3.
Mtume alikuwa akisali huku amevaa viatu, Al
Mughira alijaribu kumkumbusha Muhammad hasa pale alipomwona anatawadha juu ya
viatu na kuingia navyo msikitini, hivyo Mughira akasema “Ewe Mtume wa Allah
umesahau’’ Mtume akajibu kumwambia Al Mughira akisema “wewe ndiwe uliye sahau
kwa maana hivi ndivyo alivyo niamuru Mungu.
Kama mtume aliambiwa asali na viatu, mbona
wewe mwislamu unatoa vyatu?. Je wewe unamfuata nabii yupi?. Mafundisho ya kutoa
viatu umeyapata wapi?
SAHIH
MUSLIM VOL 1 HADITHI 1127. UK 277.
Abdullah bin Shakhkhir kuwa alikuwa akisali
na mtume wa Allah, (katika msikitini) kisha akamwona akitema mate na kuyafuta
kwa kiatu.
Kunaruhusiwa kusali huku umevaa viatu.
SAHIH
MUSLIMU VOL 1 HADITHI 1129
Sa’d bin Yazid (Abu mslama) akimliza mtume
Anas bin Malik. Je mtume wa Allah alikuwa akisali na viatu vyake, Anas akajibu NDIYO.
IBADA YA KWELI SI KUVUA VIATU BALI NI
KUMUABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI BALI SI KATIKA KUVUA VIATU.
Asiliana nasi kupitia yesundiyenjia@hopefm.org
No comments:
Post a Comment