Friday 20 December 2019

JE, ISA BIN MARYAMU NDIYE YESU KRISTO?

Utangulizi
Kwa miaka mingi sasa imekuwa ni kawaida kuwasikia waislamu wakifundisha jamii kuwa ‘Isa bin Maryam’ Kama Qurani inavyofundisha ndiye “Yesu Kristo”. Mafundisho haya hivi sasa yanaendeshwa kwa mtindo wa kulinganisha aya za Biblia na Qurani. Wahadhiri wa dini ya kiislam wanaendesha Mihadhara ambayo imeenea sana duniani na hasa zaidi katika nchi za Africa ya Mashariki na Kati (East and Central). Wahadhiri hao pia huchapisha vijarida na kurekodi kanda za audio na video, ambazo zimesababisha baadhi ya Wakristo waamini kuwa Isa Bin Maryamu ndiye Yesu Kristo. Swali la msingi kwa Wakristo wote; je, ni kweli kuwa Isa bin Maryamu ndiye Yesu Kristo? Nakusihi fuatilia somo hili.
SEHEMU KUU NANE ZA SOMO HILI
1. Hoja zinazotumika na Waislamu kusema Isa ndiye Yesu
2. Je, mama wa Isa ndiye wa Yesu?
3. Maama ya jina Isa
4. Maama ya jina Yesu
5. Je, kuzaliwa kwa Yesu ni sawa na Isa?
6. Je, Isa bin Mariamu ni mwana wa Mungu?
7. Je, mamlaka ya Isa na Yesu ni sawa?
8. Ikiwa Yesu ndiye Isa je, Isa.
9. Ujue umuhimu wa kumwamini Bwana Yesu
1. Hoja zinazotumika na waislamu kusema Isa ndiye Yesu.
Quran 3:45 (Kumbukeni) waliposem malaika. ‘Ewe Maryamu Mwenyezi Mungu anakupa habari njema za (kumzaa moto bila mume bali hali kwa kutamka) Neno tu litokalo kwake (la kumwambia zaa ukazaa pasina kuingiliwa) jina lake ni Masihi Isa mwana Maryamu, mwenye hishima kaitka dunia na ahera na miongoni mwa waliopelekwa mbele na Mwenyezi Mungu.
Marko 6:3-4
Huyo si Yule seremala, mwana wa Mariamu na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake. Yesu akawaambia ‘Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jamaa zake na nyumbani mwake.
Hapa Waislamu wanasema kana vile Qurani inavyofundisha jina la mama wa Isa ni Mariamu kadhalika Biblia inafundisha jina la mamake Yesu ni Mariamu. Hivyo wanasema kuwa Yesu ndiye Isa. Soma pia Mathayo 1: 18-21 na Yohana 2:1.
2. Hoja ya pili Isa ni Mtume wa Allah kwa Waisraeli
Qurani 4: 171: Enyi watu wa kitabu misipindukie mipaka katika dini yenu, wala msiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila yaliyo kweli. Masihi Isa bin Maryamu ni Mtume waMwenyezi Mungu…
Hapa tunaona kuwa Qurani imemtaja Isa kuwa ni ntune, je, n=mtume kwa akina nani? Endelea kusoma aya hizi katika Qurani.
Qurani 61: 6 – Na (wakumbushe) aliposema (Nabii) Isa bin Maryamu (kuwaambia mayahudi) enyi wana wa Israili! Mimi ni mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu. Nisadikishaye yaliyo kuwa kabla yangu kaitka Taurati. Na kutoa habari njema ya mtume atakeayewajia nyuma yangu ambaye jina lake litakuwa Ahmad…Soma pia katika Qurani 3: 49.
Ayah ii inathibitisha kuwa Isa ni mtume kwa Waisraeli. Je, Yesu ni mtume kwa akina nani? Waislamu wanaoendesha mihadhra pia husoma aya hizi za Biblia.
Waebrania 3:1- Kwa hiyo ndugu watakatifu wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtakafarini sana mtume na kuhani mkuu wa maungamo yetu Yesu.
Mathayo 15:24 – Akajibu, akasema, ‘Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli’.
Kwa hivyo kama Qurani inavyofundisha kuwa Isa mwana wa Maryamu ni mtume kwa Waisreali ndivyo Biblia inafundisha kuwa Yesu ni mtume kwa waisraeli hivyo basi Isa ndiye Yesu. Hivi ndibyo wahadhiri wa dini ya Uislamu wanavyoifundisha jamii. Je, hoja hii ni sahihi nitajibu mbele:-
3. Hoja ya tatu
Isa bin Maryamu alifanya miujiza
Qurani 5: 110 (kumbukeni tena) mwenyezi Mungu atakaposema, Ewe Isa mwana wa Maryamu kumbukeni neema yangu juu ya mama yako. Nilipokusaidia kwa (kukupa kuwa na wewe) Roho takatifu (Jibrili), ukazumgumza na watu (maneno ya nafuu) katika utot (wako) na katika utuuzima (wako). Na (kumbuka) nilipokufundisha kuandika na (nikakupa) hikima, Torati na Injili na ulipotengeneza kwa undongo sura za ndege kwa odhini yangu, na ulipo waponesha vipofu na wenye mbalanga kwa ihini yangu, na ulipowatoa (baadhi ya) wafu (makaburi mwao) kwa idhini yangu, na nilipokuzuilia wana wa Israeli (wasikudhuru) ulipowafikia kwa joha zilizo wazi; wale walio kufuru miongoni mwao wakasema: Haya si chochote ila ni uchawi dhahiri.
Waislamu wanasem huu ni ushahidi wakutosha kwani Allah anasema Isa alifanya miujuza mingi hii.
Isa aliponyesha vipovu ndiye…..Yesu aliponyesha vipovu Mk 10:46-52
Aliwafufua wafu makaburi ndiye……. Yesu alifufua mwau Mk 5:21-43
Aliwaponyesha wenye mbalanga ndiye…Yesu aliponya Ukima -Lk 17:1
Wahadhiri wa kiislamu wanasema kama vile Qurani invyosimulia kuwa Isa amefanya miujiza mingi, ndiyo Biblia inavyofundisha hivyo Yesu ndiye Isa isitoshe wanasema hive: - Isa ibin Maryamu ni Nabii, Suratul 4:171, kadhalika Biblia inafundisha kuwa Yesu ni Nabii, Yohana 6:14, Yohan 7:40, Luka 13:33; 24:19, Marko 6:4, na Mathayo 13:57. Kwa wastani Biblia inafundisha uwa Yesu ni Nabii mare 12. Vile vile wahadhiri wa Kiislamu wanafundicha y kwamba Isa ni Neno la Kiarabu, katika kiingreza Jesus na kwa Kiswahili ni Yesu. Kupitia vigezo hivi baadhi ya Wakristo wameshawishika kuamini kuwa Isa ndiye Yesu. Lakini, lazima tuzichunguze hizi hoja moja baada ya nyingine ili tujue ukweli.
2. Je, Mama wa Isa ndiye wa Yesu Kristo
Hapo awali tumeona kuwa mama wa Isa anaitwa Maryamu, Surah 3:45 na pia mama wa Yesu anaitwa Mariamu Mathayo 1: 18-21, Marko 6: 3-4 lakini kufanana kwa majina hakuwezi kamwe kumaanisha kuwa ni mtu mmoja, kwani walio na jina hilo ni wengi. Biblia inatufundisha hivi.
Yohana 19:25 – Na penye Msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama, Mamaye, na ubu la mamaye Mariamu wa Klopa na Mariamu Magdalena.
Hapa tunaona Mariamu watatu. Ili kutambua tofauti baina ya Mariamu mama wa Isa na mama wa Yesu, lazima tulinganishe ujumbe wa Qurani na Biblia. Qurani inasimulia kuhusu baba na kaka wa Mariamu mama wa Isa hivi.
Suratul 66:12 – Na Maryamu motto wa Imrani aliyejihifadhi nafsi yake na tukampuliza humor oho yetu, (inayotokana na sisi) na akayasadikisha maneno ya mola wake, na vitabu vyake; na alikuwa miongoni mwa wanyenyekevu (wakubwa).
Surah 19:28 – Ewe dada yake Haruni. Baba yako hakuwa mtu mbaya. Wala mama yako hakuwa hasharati.
Hapa tunaona kuwa Maryamu mama wa Isa, baba yake ni Imrani na kaka yake aliitwa Haruni. Tusomapo Biblia inatueleza kuwa Amrani aliwazaa hawa:-
Hesabu 26:59 – Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi binti wa Lawi, ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amram Haruni, na Musa, na Miriamu umbu lao.
Pia soma 1 Nyakati 6: 1-3 na Kutoka 6:20.
Huyo Amrani aliishi miaka mingi kabla ya Yesu na, tena ametokana na kizazi cha Lawi motto wa watu wa mzee Yakobo. Mwanzo 29:34; Kutoka2:1-10
Ikiwa Mariamu wa Qurani baba yake ni Imrani basi atakuwa ameishi miaka 1 500 kabla mama yake Yesu hajazaliwa!
Je, Mariamu mama wa Yesu ametokana na kizazi gani?
Tunaposoma Biblia tunaona kwamba Yesu anaitwa mwana wa Daudi Mathayo 1:1; Marko 10:47 na Luka 1:27, 32, ndiyo maana pia Yesu anaitwa Simba wa Yuda Ufunuo 5:5. Hivyo basi ukoo aliyetoka Yusufu na Mariamu wa Yesu ni mmoja.
3. Maana ya jina Isa
Ni jambo la kawaida sana jina au majina kuwa na maan. Mfano majina haya y kiarabu yana maana hizi: Muhammad, linamaanisha mwenye kushukuriwa, Abdalla ni Mtumwa wa Allah; Abu-Bakar maana yake ni Baba wa bikira; Abu Huraira ni baba wa Mapaka. Aidha majina ya Kiebrania nayo pie yana maana. Malaki ni mtumishi au Mjumbe wa Yehova, Isaya ni Wokovu wa Yehova; Ezekiel inamaanisha Mungu hutia nguvu, Daniel – Mungu ni hakimu wangu.
Jina Isa maana yake ni hii
Katika Qurani yenye jumla ya juzuu 30; Surah 114; aya 6236; maneno yenye kutamkia 76,440; herufi 322,373; jina Isa linatamkwa lisa au Aysi limetajwa mara 25. Isa pia ameitwa masihi mara 93. Lakini tunaposoma Qurani iliofarsiriwa na Imam Baidawi vol 1ukurasa 160 ameeleza kuwa Isa jina la Kiarabu maana yake ni Wekundu unaozidiana na weupe.
4. Maana ya jina Yesu
JINA Yesu lintokana na lugha ya Kiebrania ‘Yehoshua’ katika lugha ya Kigiriki wanasema ‘lesous’ inatamka ‘Yesous’ yaani Yesu. Katika lugha ya Kiarabu wanasema ‘Yasu’, kwa kiingereza ni “Jesus” maana yake ‘Bwana anaokoa au Bwana ni Mwokozi’ Isaya 43:6, 10-11. Katika Biblia ambayo in jumla ya Sura 1189; aya 31,102; vitabu 66 – Agano la kale vitabu 39 na agano Jipya vitabu 27; neon Mwokozi kiiengereza wanasema ‘Saviour’ limetajwa mara 55. Ikumbukwe kwamba katika agano jiypa jina Yesu au Yehoshua (kwa kiebrania) limetajwa mara 1275 katika aya zipatazo 1226. Zingatia pia kuwa agano jipya lina jumla ya aya 7930 na sura 260 hivyo hapa tunaona jina Yesu maana yake ni Mwokozi na jina Isa ni wekundu uliozidiana na weupe. Kwa kuwa maana ya haya majina tofauti bila shaka Isa sio Bwana Yesu.
5. Je, kuzaliwa kwa Bwana Yesu ni sawa na Isa?
1. Taarfa za Malaika kabla ya kuzaliwa kwao, kadiri ya Qurani na Biblia.
Jibrili alivyomtokea Mama wa Isa Gabrieli alivyomtokea mama wa Yesu
-Alienda kwa Mariamu aliyekuwa msikitini Qurani 19:16-17
-Alienda kwa Mariamu aliyekuwa nyumbani kwake - Lk 1:26-28
-Mariamu mama wa Isa haijulikani aliishi kijiji kipi wala mji gani wala hata nchi haijulikani. Isitoshe Qurani inasema kuwa Jibril ndiye aliyemletea utume Muhammad asiwapelekee Mayahudi (hana kosa) Sura 2:97
-Lakini Mariamu mama yake Yesu alitokewa na malaika Gabriel akiwa katika kijiji cha Nazareti mji wa Galilaya nchi ya Israeli (Lk 1:26) Mariamu mama wa Yesu ni Myahudi.
-Jibrili hakutoa salamu kwa Mariamu mama wa Isa ila alijimithilisha kwa umbo la binadamu aliye kamili - Sura 19-17
Malaika Gabrieli alimsalimia Mariamu Mama wa Yesu – Luka 1:28
-Jibril alimwambia Mariamu kwamba mimi ni mjumbe wa mola wako ili nikupe mwana mtakatifu - Sura 19-19
-Lakini malaika Gabrieli alimwambia mama wa Yesu kuwa utachukua mimba – Luka1: 31
S-Jibrili alisema kwa Mariamu kuwa ili tumfanye motto muujiza kwa wanadamu – Sura 19: 21. Isitoshe Jibrili hakutaja jina la mwana kwa Mariamu. Bali alisema ili nikupe mwana mtakatifu.
-Malaika Gabrieli alisema kwa Mariamu mama ya Yesu kuwa motto jina lake utamwita Yesu (Luka 1:31; 2:21) Gabrieli hakusema kuwa atampa mwana Mariamu. Bali alisema, Roho mtakatifu atakujilia juu yako, yaani motto atazaliwa kwa uwezo wa Mungu.
2. Tofauti ya kuzaliwa Isa na Yesu ni hii
Isa Ibn Mariam Yesu Kristo
-Isa alizaliwa katika shina la mtemde – 19:23
-Yesu kazaliwa katika hori la kulishia ng’ombe. Luka 2:7
-Kuzaliwa kwa Isa haijulikani mimba ya mama yake ilichukua muda gani maana malaika Jibrili alisema nikupe mwana mtakatifu mara akachukua mimba na kuzaa. (19: 22-23)
-Lakini Mariamu mama wa Yesu siku zake za kuzaa zilitimia. (Luka 2:6-7)
-Qurani haionyeshi kama Isa alitabiriwa na manabii kuwa atazaliwa
-Lakini Biblia inatuthibitishia kuwa manabii walitabili kuzaliwa kwa Yesu, (Isaya 7: 14; 9:6) utabili huu ulitolewa na Nabii Isaya miaka 750 kabla ya Yesu kuja kuzaliwa nao ulitimia (Mathayo 1:18-23)
-Isa haijulikani alizaliwa katika kijiji gani wala mji, wala nchi aliyozaliwa Qurani haikueleza.
-Biblia inatujulisha kuwa Yesu alizaliwa Bethelehemu ya Uyahudi katika Mji wa Daudi umbali wa maili 5 toka kusini mwa Yerusalemu nchi ya Israeli (Lk 2:8-16). Kuzaliwa kwake mahali hapo pia ni kutimiza unabii uliotolewa na nabii Mika miaka 750-686 kabla ya kristo kuja wakati wa wafalme hawa wakitawala – Jotham, Ahaz na Hezekia wafalme wa Yuda. Yesu mwenyewe alizaliwa kama mwaka wa 4 wakati wa Mfalme Herode.
-Isa aliongea na watu akiwa mototo mchanga, na kusema kuwa yeye ni mja wa Mungu amepewa kitabu na amefanywa Nabii (Sura 19:30-33) -Yesu hakuongea na mtu akiwa mototo mchanga. Alianza kuwauliza maswali na kutoa majibu akiwa na wazee Hekaluni akiwa na miaka 12. (Luka 2: 42-49)
Hivyo tunaona kwamba tuna tofauti nyingi tu kati ya Bwana Yesu na Isa. Swali kwako mfuatiliaji je, Isa bin Maryamu ndiye Bwana Yesu Mwokozi? Tafakari.
6. Je, Isa bin Mariamu ni mwana wa Mungu?
Kama kuna jambo ambalo Allah Mungu anayeabudiwa na waislamu analitataa sana kupitia Qurani basi jambo hilo si linguine bali ni uwana wa Mungu. Allah ansema hivi.
Sura 6:101 – Yeye ndiye mwumba wa mbingu na ardhi, inamkinikaje awe na mwana, hali hana mke? Naye ndiye aliye umba kila kitu (sio baadhi yake kavizaa). Naye ni mjuzi wa kila kitu.
Quran 9:30 – Na mayahudi wanasema ‘uzeri ni mwana wa Mwenyezi Mungu’ na ‘wakristo wanasema Masihi ni mwana wa Mwenyezi Mungu’ haya ndiyo wasemayo kwa vinywa vyao (pasina kuyapima).Wanayaiga maneno ya wale walilkufuru kabla yao, Mwenyezi Mungu awaangamize. Wanageuzwa namna gani hawa?
Hili ni agizo la kutisha kwamba Wakristo na Wayahudi tuangamizwe kwa kuwa tunaamini Mungu ana Mwana, au wana, lakini Wakristo tunaoamini hivyo kwa sababu Mungu wetu:-
- Yehova alifundisha kuhusu Bwana Yesu hivi: Kutoka 4:22…Israeli ni mwanangu mimi……Mathayo 17:5……Huyu ni mwanangu mpendwa wangu….
- Malaika wa Mungu alisem hivi.
Luka 1:30-31, 35 – Malaika akamwambia usiogope Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama utachukua mimba na kuzaa motto mwanamume; na jina lake utmwita Yesu. Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kuvuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu Mwana wa Mungu.
Hiyow Isa siyo Mwana wa Mungu lakini Yesu ni mwana wa Mungu. Kwa hivyo Yesu siyo Isa.

No comments:

Post a Comment