Friday 11 October 2013

MAANA HALISI YA KANISA



KANISA
Kanisa ni nini? Je Kanisa ni jengo? Je, ni mahali watu wanakusanyika ili kuabudu Mungu? Au Kanisa ni watu-Waumini wanaomwamini na kumfata Yesu? Jinsi tunavyoelewa kanisa ni kitu cha muhimu kwa kutusaidia kujua jinsi ya kuishi na kuenenda katika imani yetu kuu.
Baadhi ya watu wanaamini kwamba neno Kanisa limetajua mara ya kwanza na Bwana Yesu katika aya ifutayo:
Mathayo 16:16–18
Simoni Petro akajibu akasema wewe ndiwe Kristo mwana wa Mungu aliye hai Yesu akajibu akamwambia heri wewe Simon Bar Yona kwa sababu mwili na damu hazikukufunulia haya bali baba yangu aliye mbinguni nami nakuambia wewe ndiwe Petero na juu ya Mwamba huu nitalijenga kanisa langu wala milango ya kuzimu haitalishinda.”
 Maana halisi ya kanisa
Neno “Kanisa” kama linavyo elezwa na maandiko matakatifu, limetokana na neno la kigiriki ambalo ni ekklesia ambalo maanake halisi ni “kusanyiko” na “kuwaita watu” au “wale ambao wameitwa” kwa kifupi tu ni kwamba Kanisa ni mwili wa waumini ambao wameitwa au wamesikia mwito kutoka ulimwenguni na Mungu ili waishi kama watu wake chini ya himaya au mamlaka ya Kristo Yesu (Waefeso 1:22-23)
Baadhi ya maadui wa injili na hasa waislamu mara nyingi hua wanauliza na kujenga maswali yasio faa juu ya Kanisa ima kwa ujinga au kwa ujeuri tu ili ionekane kwamba Kanisa ni kitu hakipo au ni kitu kisicho faa. Baadhi ya hoja wazijengazo kinyume na injili tukufu ni haya:

HOJA ZA KANISA
1.      Wapi aya Yesu kaingia Kanisani?      
2.      Kanisa imejengwa juu ya shetani Mathayo 16:8
3.      Eti Kanisa ni kiti cha enzi cha shetani Ufunuo 2:12-13.
4.      Kanisa ni nyumba ya kileo- Mithali 9:1
5.      Kanisa ni nyingi gani ndio bora?
6.      Kanisa ni nyumba ya mafarakano 1 Korinthians 11:7 (No place for disorder 1Cor 14:33).

Kanisa ni mwili wa Yesu Wakolosai 1:18, 1:24
Yesu ndiye kichwa cha Kanisa Waefeso 4:23
Tuko na Kanisa la ukweli na la uongo
Mfano wa kanisa la uongo 2 petero 2:1
Mfano wa Kanisa la ukweli ni gani? Waebrania 12:24

JINSI YA KUKUA SEHEMU YA KANISA
Mtu hufanyika sehemu ya kanisa pale anapo mkubali Bwana Yesu kukua Bwana na mwokozi wa maisha yake.
KUSUDI KUU LA KANISA NI GANI?
Kusudi kuu la Kanisa lipo mara mbili kwanza ni Kanisa huja pamoja (hukusanyika) na kusudi la kuhimizana na kujenga katika masala ya kiroho ili mtu akomee (Waefeso 4:13). Kanisa hufikia na kusambaza upendo na injili kuu ya Mbwana Yesu Kristo kwa wale wasio amini ulimwenguni (Mathayo 28:18-20). Hii ndio iitwayo Mwito mkuu hivo basi kusudi la Kanisa ni kuhudumia waumini na wasio waumini.
1 Wakorintho 12:27, Kanisa ni mwili mmoja
(Mw. ZABLON NYONJE).


No comments:

Post a Comment